Klabu ya soka Newcastle United imemsajili kiungo wa kimataifa wa Uingereza Andros Townsend kwa dau la pauni milioni 12 akitokea Tottenham Hotspur.
Townsend mwenye umri wa miaka 24 amesaini mkataba wa miaka mitano kukitumikia kikosi cha Newcastle chini ya meneja wake Steve Mclaren.
Kiungo huyo amecheza michezo mitatu ya msimu huu akitokea benchi huku akiondolewa katika kikosi kilichokua kinashiriki michuano ya Europa ligi baada ya kugombana na kocha wa viungo Nathan Gardiner.
Townsend alijiunga na kituo cha michezo cha Spurs akiwa na miaka nane na alianza kukitumiki kikosi cha kwanza katika msimu wa 2013-14.
0 maoni:
Chapisha Maoni