January 28 klabu ya soka ya Chelsea ya Uingereza imerudi tena kwenye headlines, safari ni ule muendelezo wa stori zao za usajili, Chelsea ambayo imeingia kwenye headlines za usajili mara kadhaa sasa toka dirisha dogo la usajili lifunguliwe. Tayari inatajwa kukamilisha mpango wa kumsajili kwa mkopo Alexandre Pato.
Chelsea ilikuwa inahusishwa kutaka kumsajili kwa mkopo mchezaji wa kimataifa waBrazil kutokea klabu ya Corinthians, msimu uliopita Pato alichezea kwa mkopo klabu ya Sao Paulo ya kwao Brazil akitokea Corinthians iliyomsajili kwa euro milioni 15 akitokea AC Milan, kwa sasa atajiunga na Chelsea kwa mkopo. Pato tayari ametuaLondon kukamilisha dili hilo.
“Nipo hapa kutimiza ndoto zangu, Chelsea ni nyumbani na ninafuraha kuitumikia, kiukweli nina furaha sana, nataka kukutana na wachezaji wenzangu wapya na kuanza kuzoea mazingira haraka” >>> Pato
0 maoni:
Chapisha Maoni