Diego Costa akishangilia ushindi.
Mshambuliaji
wa Chelsea, Diego Costa ameisaidia klabu yake kuibuka na ushindi wa
goli moja kwa bila mbele ya wapinzani wao wa kutokea jiji moja la
London, Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza, mchezo
uliochezwa katika uwanja wa Emirates unaomilikiwa na Arsenal.
Costa
alifunga goli hilo katika dakika ya 23 baada ya kuunganisha mpira mrefu
uliopigwa na beki wa klabu hiyo, Branislov Ivanovic goli lilidumu kwa
dakika zote 90 za mchezo huo hadi mwamuzi Mark Clattenburg anapuliza
filimbi ya kumalizika kwa mchezo huo.
Aidha
Arsenal ilimaliza mchezo huo ikiwa na wachezaji 10 pekee uwanjani baada
ya beki wa timu hiyo, Per Mertesacker kuonyeshwa kadi nyekundu katika
dakika 18 ya mchezo huo baada ya kumchezea vibaya mshambuliaji wa
Chelsea, Diego Costa.
Baada
ya matokeo hayo Arsenal imebaki na alama zake 44 huku ikiwa katika
nafasi ya 3 nyuma ya Manchester Citty na Leister City na Chelsea
ikipanda kwa nafasi moja kutoka nafas ya 14 hadi 13 huku ikiwa na alama
28.
Matokeo
mengine ya Ligi Kuu ya Uingereza iliyochezwa jana Jumapili, Januari 24
ni Everton iliyowakaribisha Swansea City na mchezo huo kumalizika kwa
Swansea kuibuka na ushindi wa goli mbili kwa moja, magoli ya Swansea
yakifungwa na Gylfi Sigurdsson dakika ya 17 na Andre Ayew katika dakika
ya 34 huku beki wa Swansea Jack Cork akijifunga goli la kufutia machozi
kwa Everton katika dakika ya 26.
Diego Costa (blue) akifunga goli.
Diego
Costa (blue) akimtoka beki wa Arsenal, Hectoe Bellerin (nyekundu)
katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza kati ya Arsenal na Chelsea.
Kiungo wa Arsenal, Mesut Ozil akiwania mpira na Eden Hazard wa Chelsea.
Kiungo wa Arsenal, Metheu Flamini (nyekundu) akiwania mpira na kiungo wa Chelsea, William (blue).
Refa wa mchezo huo, Mark Clattenburg akimwonesha Mertesacker kadi nyekundu.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger akilalamika kwa refa wa mchezo huo, Mark Clattenburg.
Per Mertesacker akiwa ameketi na Oliver Giroud baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu.
0 maoni:
Chapisha Maoni