Shirikisho la Soka nchini (TFF) lipo katika mchakato wa kuanzisha Ligi Kuu ya Wanawake itakayoanza muda wowote mwaka huu.
Hayo yalisemwa jana na Rais wa TFF, Jamal Malinzi wakati wa mkutano mkuu
wa shirikisho hilo uliofanyika kwenye Hoteli ya Naivera jijini Tanga.
Malinzi alisema kuwa mbali na ligi hiyo, pia mwaka huu itaanzishwa Ligi
Kuu ya vijana chini ya miaka 20 na kufuta mashindano ya Kombe la Uhai na
tayari mchakato wa kupata wadhamini kwa ajili ya ligi hizo mbili
umeanza.
“Mara kadhaa tumekuwa tukipigiwa kelele juu ya ligi ya wanawake, ambayo
hatujawahi kuwa nayo, ila msimu huu kwa maana ya msimu ujao ligi hiyo
itakuwa imeanza pamoja na ligi ya vijana hivyo hatutakuwa na michuano ya
Kombe la Uhai,” alisema Malinzi Malinzi.
- Blogger Comment
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
0 maoni:
Chapisha Maoni