Wakati watani zao wa jadi Yanga wamemaliza kucheza mchezo wao wa kwanza wa raundi ya pili katika michuano ya klabu bingwa Afrika dhidi ya APR ya Rwanda kwa ushindi wa goli 2-1 March 12, Simba wao wameshuka dimbani March 13 kuendeleza harakati zao za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara.
Simba wameshuka dimbani kucheza dhidi ya klabu ya wajelajela wa Mbeya Tanzania Prisons, katika mchezo wao 23 wa Ligi Kuu Tanzania bara. Simba waliingia uwanjani kuhakikisha wanapata point tatu ili waendelee kuwa katika nafasi nzuri ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara.
Hata hivyo licha ya jitihada kubwa kuoneshwa ndani ya dimba la uwanja wa Taifa naTanzania Prisons za kuataka kutoa sare, hazikuzaa matunda, kwani Simba ilifanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 kupitia kwa Awadh Juma dakika ya 88. Kwa matokeo hayoSimba anaendelea kuongoza Ligi akiwa na jumla ya point 54 akifutiwa na Yanga aliyemzidi point 3 na michezo miwili.
0 maoni:
Chapisha Maoni