Muda mfupi baada ya filimbi ya mwisho kupulizwa kwenye uwanja wa Nou Camp, hiyo picha Ilianza kusambazwa kwa kasi na ma-star wa Real Madrid pamoja na clab kwa ujumla ikionesha wachezaji wakiwa pamoja wanasherekea ushindi wao wa magoli 1-2 dhidi ya Barcelona kwenye vyumba vya bubadilisha nguo.
Picha za kusherekea ushindi hasa kwenye mechi kubwa na muhimu sikuizi imekuwa ni jambo la kawaida. Zamani haikuwa kawaida kwa wachezaji kusherekea pointi tatu kama wanavyofanya wachezaji wa leo, wachezaji wa zamani walikuwa wakisherekea zaidi pale timu yao inapofanikiwa kutwaa ubingwa.
Sikuhizi picha imekuwa ni kawaida kama vile sehemu ya maisha kuliko miaka michache ya nyuma, ma-star wa Real Madrid wote wana account kwenye mitandao ya kijamii na wanahitaji ku-update kila wakati kwa ajili ya kuwonesha mashabiki wao kile wanachokifanya kwa wakati husika kama wachezaji wakubwa duniani.
Katika picha iliyopigwa baada ya kutoa kichapo kwa Barcelona, Ronaldo ndiyo amekuwa kivutio kwa mashabiki wengi.
Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Ureno ni mchezaji pekee wa Madrid ameonekana kwenye picha hiyo akiwa amevaa chupi tu!
Kiuhalisia, kwenye picha hiyo Ronaldo ndiyo mchezaji maarufu zaidi duniani kuliko wengine. Unaweza ukaona namna ambavyo amejaribu kufanya kitu ambacho bado kitamtofautisha na wengine na kuendelea kumuweka kwenye soko.
Lakini kulingana na matokeo ambayo timu yake iliyapata uwanjani dhidi ya Barcelona huku akiwa ameweka nyavuni bao moja lililoisaidia timu yake kupata ushindi, utamlaumu Ronaldo kwa hicho alichokifanya?
0 maoni:
Chapisha Maoni