Baada ya kupiga bao wakai England ikitoka nyuma na kuchapa Ujerumani kwa bao 3-2 wiki iliyopita, Kane amerudia mambo kama hayo wakati Spura ikichuana na Liverpool kwenye uwanja wa Anfield.
Ikiwa ni mechi muhimu kwa Tottenham ambao wako kwenye mbio za kuwania ubingwa wa Premier League, Kane alitupia kambani bao la kusawazisha dhidi ya Liverpool ambao walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na Philippe Coutinho.
Goli hilo limemuongezea Kane idadi ya magoli na kufikisha magoli 22 kwenye ligi msimu huu. Hiyo ni rekodi mpya ndani ya klabu ya Tottenham kwenye Premier League ya mshambuliaji kufunga magoli 22 ndani ya msimu mmoja.
Gareth Bale na Teddy Sheringham (ametimiza miaka 50) walikuwa wanashikilia rekodi ya wachezaji waliowahi kufunga magoli mengi kwenye klabu hiyo ndani ya msimu mmoja, walifunga magoli 21.
Angalia picha ya graphics ikionesha rekodi mpya iliyowekwa na Harry Kane baada ya kufunga bao kwenye mchezo dhidi ya Liverpool.
0 maoni:
Chapisha Maoni