MOHAMED ELNENY AWEKA REKODI EPL 2015-16

Elneny 2
Mohamed Elneny ameweka rekodi mpya kwenye Premier League wakati Arsenal ikicheza mchezo wa ligi dhidi ya Watford siku ya Jumamosi.
Wakati mashabiki wengi wa soka wakiamini Leicester au Tottenham watatwaa taji la ligi msimu huu, Arsenal wameshinda mchezo wao kwa kuichakaza Watford kwa mabao 4-0 wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani Emirates.
Kinda wa Arsenal Alex Iwobi ameendeleza makali yake baada ya leo kupika bao la kwanza ambalo lilifungwa na Alexis Sanchez kabla ya kijana huyo mwenye miaka 19 hajapachika bao lake la pili kwenye EPL.
Shuti la Bellerin lililokuwa ‘deflected’ mwanzoni mwa kipindi cha pili likaendelea kiweka mbele Arsenal wakati Theo Walcott akitokea benchi akamaliza mchezo kwa kupiga bao la nne.
Mohamed Elneny kwa mara nyingine amecheza dakika zote 90 za mchezo kwenye mechi kali, mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri ameweka rekodi mpya kwenye mchezo huo wa Premier League.
Elneny amefanikiwa kupiga pasi 121 kwenye mchezo wa leo akiivuka rekodi ya mchezaji mwenzake Santi Cazorla aliyekuwa amepiga pasi nyingi kwenye mchezo dhidi ya Newcastle mwezi August.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Chapisha Maoni