Liverpool yatoka sare na Dortmund


Divock Origi aliifungia Liverpool bao muhimu la ugenini katika mechi yao ya raundi ya kwanza ya nusu fainali dhidi ya Borussia Dortmund ya Ujerumani.Borussia DortmundBorussia Dortmund
Bao hilo la mshambulizi huyo wa Ubelgiji, lilikuwa pigo kubwa kwa kocha Jurgen Klopp, hasa kwa kuwa Origi alikuwa mchezaji wa zamani wa klabu hiyo.
Hata hivyo kipa wa Dortmund Roman Weifenfeller, aliokoa mkwaju mwingine wa Origi kabla ya Mats Hummels kusawazishia wenyeji.
Juhudi za Dortmund za kufanya mashambulio zaidi katika lango la Liverpool hazikufua dafu pale vijana hao wa Uingereza walipojizatiti na kuzima mashambulio hayo.
Hata hivyo matokeo hayo yalikuwa mema kwa Dortmund, ambayo inapigiwa upato kutwaa kombe hilo la Europa.
Katika mechi zingine Athletico Bilbao walinyukwa mabao mawili kwa moja mbele ya mashabiki wao na klabu ya Sevilla.
Sporting Braga nao walivishwa mabao mawili kwa moja na wageni wao Shaktar Donetsk huku Villarreal ikiwika nyumbani dhidi ya Sparta Prague. Villarreal iliibuka na ushindi wa magoli mawili kwa moja.
Mechi za awamu ya pili ya kombe hilo zinatarajiwa kuchezwa baada ya majuma mawili.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Chapisha Maoni