Usiku wa Jumanne, kikosi cha Manchester United U21 kiliichapa Tottenham Hotspur U21 kwa magoli 3-2 na kuchukua ndoo ya Premier League. Kikosi hicho kimeendelea kudhihirisha kwamba Manchester United inazalisha vijana wengi wenye vipaji vya hali ya juu.
Vijana hao walishinda kwa style ya aina yake, wakijihakikishia kutwaa taji hilo dakika ya 94 kupitia kwa mlinzi wao wa pembeni Guillermo Varela. Hata hivyo pambano hilo halikuwa rahisi kwao kwasababu waliongoza kwa magoli 2-0 mapema lakini walisawazishiwa na kikosi cha Spurs na matokeo kuwa 2-2. Kisha kupata bao la ushindi dakika za lala salama.
Mchezaji aliyekuwa kivutio kwenye game hiyo ni M-brazil Andreas Pereira. Kijana ambaye alionesha uwezo mkubwa kutokana na kufunga bao kwa kutumia uwezo wa hali ya juu kabla ya shuti lake jingine kugonga mwamba.
0 maoni:
Chapisha Maoni