Matumaini ya kilabu ya Kenya Gor
Kahia kuendelea katika kombe la vilabu bingwa Afrika CAF yalimalizwa
siku ya jumamosi baada ya kupoteza mechi ya marudiano ya mchuano huo
ugenini .
Gor Mahia walilazwa kwa bao 1-0 na kilabu ya CnaPs nchini Madagascar.Mabingwa hao wa Madagascar walilipiza kisasi baada ya kupoteza kwa K'ogalo katika awamu hiyo hiyo msimu uliopita kwa kujipatia jumla ya mabao 3-1.
K'Ogalo ilipoteza raundi ya kwanza dhidi ya CnaPs kwa mabao 2-1 nyumbani Nairobi.
Kiungo wa kati wa kilabu hiyo ya Madagascar ,Martin Njiva Rakotoharimalala alifunga bao hilo muhimu kunako dakika ya 28 katika mechi iliochezwa katika uwanja wa Rabemananjara huko Mahajanga.
Kocha wa kilabu hiyo Frank Nutall kwa mara nyengine alimuanzisha nahodha wa kilabu hiyo Jerim Onyango katika lango badala ya kipa wa Harambee Stars Boniface Oluoch huku kiungo wa kati Khalid Aucho na mshambuliaji mpya Jacob Keli wakianza kama wachezaji wa ziada.
0 maoni:
Chapisha Maoni