Mabondia
Francis Miyeyusho kushoto na Nassibu Ramadhani wakitambulisha mpambano
wao utakaopigwa siku ya sikukuu ya pasaka katika uwanja wa ndani wa
taifa katikati ni kiongozi wa ngumi Antony Rutta Picha na SUPER D BOXING NEWS
Kiongozi
wa mchezo wa masumbwi nchini Antony Rutta katikati akiwainua mikono juu
kuwatambulisha mabondia Francis Miyeyusho kushoto na Nassibu Ramadhani
mbele ya waandishi wa habari Dar es salaam juzi kwa ajili ya
kutambulisha mpambano wao wa pasaka katiku uwanja wa ndani wa taifa
Picha na SUPER D BOXING NEWS
Mabondia
Francis Miyeyusho kushoto na Nassibu Ramadhani wakitunishiana misuli
mbele ya waandishi wa habari katikati ni kiongozi Antony Ruta wa pili
kushoto ni Dei Miyeyusho na mwingine ni kocha Christopher Mzazi wakati
wa kutangaza mpambano wa mabondia hawo siku ya Pasaka Picha na SUPER D BOXING NEWS
Na Mwandishi Wetu
MABONDIA
Francis Miyeyusho na Nassibu Ramadhani wamesaini mkataba wa makubaliano
wa kuzipiga siku ya sikukuu ya Pasaka katika uwanja wa ndani wa taifa
jijini Dar es salaam
Akizungumzia
mpambano uho mratibu wa mabambano hayo Rajabu Mhamila ‘Super D’ amesema
kuwa amewasainisha mabondia hao kwa kuwa viwango vyao vipo juu sana
katika kipindi hiki na ndio mpambano mkali utakaokuwa wa kufungua mwaka
2016
Aliongeza
kwa kusema mbali na mpambano huo siku hiyo pia kutakuwa na mapambano
mengine ya kukata na shoka ambapo mabondia mbalimbali watazipiga
siku hiyo.
Mohamed
Matumla atavaana na Cosmas Cheka wakati mabondia Mada Maugo atavaana na
Abdalla Pazi katika mpambano wa nani zaidi kati yao pia bondia Vicent
Mbilinyi atavaana na Mwinyi Mzengela na Pius Kazaula wa Morogoro
atamenyana na Seba Temba.
Super D
amewataka wapenzi wa mchezo wa masumbwi kujitokeza kwa
wingi ili kushudia mpambano huo ambao unatarajiwa kuwa na msisimko wa
aina yake, vilevile mabondia hao wamepanga kuanza ngumi hizo mapema ili
wapenzi wafurahie mchezo huo mapema na kurudi majumbani na kujumuika
na familia zao katika sikukuu hiyo hivyo ameomba mashabiki kufika mapema
ili ngumi nazo zianze kwa wakati muafaka na kumalizika mapema.
0 maoni:
Chapisha Maoni